Video and Shared space ads

Tuesday, April 10, 2012

KANUMBA THE GREAT (R.I.P)



Kama barafu juani umeyeyuka,
Kama mshumaa kwenye upepo umezimika,
Jumamosi alfajiri umetutoka,
Kanumba the great tutakukumbuka.

Nje ya mipaka ya nchi umetuwakilisha,
Nollywood mpaka Hollywood umefika,
Bendera ya Tanzania kuitangaza,
Kanumba the great tutakukumbuka.


Kifo chako kimekuwa cha utata,
Mashabiki wako ukweli twautaka,
Machozi yamekuwa yakitutoka,
Kanumba wetu bado twamtaka,
Daima tutakukumbuka Kanumba the great.

Tarehe 10/4/2012 leaders club tutakuaga,
Filamu zako zaidi ya arobaini ni mfano wa kufuatwa,
Kwenye nyumba yako ya milele jioni tutakulaza,
Mioyoni mwetu huzuni umeijaza,
R.I.P Kanumba the great.
 Imeandaliwa na Ally Bukuku/Buchicks

No comments:

Post a Comment