Video and Shared space ads

Sunday, March 25, 2012

SIO LINGINE BALI KUTAKA KUKUTULIZA


Kwanza naanza kwa kutambaza,
Maneno matamu kukuliwaza,
Moyo wako kuusuuza,
Sio lingine bali kutaka kukutuliza;

Wengi wamekuliza,
Machoni wakakutuliza,
Moyoni wakakupoteza,
Fikirani mwao hukuingizwa,
Sina lingine bali kutaka kukutuliza;

Ahadi naiwekeza,
Kapuni naitupia,
Ubani ntajifukiza,
Marashi ntakunyunyiza,
Kwa pamoja tutanuiza,
Sio lingine bali kutaka kukutuliza;

Mapenzi yako ntayatukuza,
Uzuri wako utaniliwaza,
Furaha ntakujaza,
Penzi lako ntalitunza,
Sio lingine bali kutaka kukutuliza;

Najua wengi wanakutongoza,
Majigambo kujijaza,
Uzuri wao kujikweza,
Pesa zao kuzitandaza,
Ila tofauti yetu itajitokeza,
Ni wewe tu wakuichomoza,
Sio lingine bali kutaka kukutuliza;

Nashkuru kunipongeza,
Furaha ushaanza kuijaza,
Maneno matamu umeyawekeza,
Kwa uweza wa sauti yako ulipo ni chombeza,
Wakati twajuana kwa mara ya kwanza,
Kunieleza wazi kuwa ushawabeza,
Na mimi ndio wa pekee moyoni naekupendeza,
Sio lingine bali kutaka kukutuliza.

Imeandaliwa na Baharia


No comments:

Post a Comment