Video and Shared space ads

Friday, March 23, 2012

CHA MWIKO UTAKIONA


Ukumbini najongea, Kwa kitambo nimemezea,
Mengi nimejionea, Baharini yalojitokezea,
Dunia imejichokea, Kwa binadamu ni mazoea,
Lamba lamba kama asali, cha mwiko utakiona;

Ujio huu sio wa ukali, bali kwa kile nlichokiona,
Uvumi umekuwa kauli, Kwamba sicho wanachokinena,
Wewe umsafi kiakili, mpaka kimwili unajivuna,
Lamba lamba kama asali, cha mwiko utakiona;



Nakuasa wewe baba wawili, Mwenye tamaa za kimwili,
Hivi kweli unaakili, Watoto wa wenzio kuwaingilia kimwili,
Usijione unamali, Tukikuchoka tutakuletea timbwili,
Lamba lamba kama asali, cha mwiko utakiona;

Chezea wa wenzako, Ila siku watu watakuweza,
Siombei mabaya kwako, Bali nakupa ili kukujuza,
Siku tutakukalia kitako, Kama ulezi tutakutandaza,
Lamba lamba kama asali, cha mwiko utakiona;

Yangu mimi namemaliza, Ujumbe umeupata,
Kama shari ishaanza, Kwa kweli utaipata,
Sinashaka utajilaza, Ukitafakari yatayokupata,
Lamba lamba kama asali, cha mwiko utakiona.


Imeandaliwa na Baharia


No comments:

Post a Comment